Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea ,anawatangazia wamiliki wote wa ardhi ,kuwa kuna zoezi la uhakiki wa taarifa za Wamiliki wa ardhi Nchi nzima kuanzia tarehe 1.7.2021 hadi tarehe 30.9.2021.
Watakaohusika katika zoezi hili, ni Wamiliki wote wenye Hati Miliki, wenye Barua za toleo (letter of offer) au wanaomiliki kwa kutumia Leseni za Makazi.
Zoezi hilo la uhakiki wa umiliki litafanyika katika ofisi za Ardhi na Mipango Miji Manispaa ya Songea chumba no 36, kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
Kila Mmiliki wa ardhi anahitajika kuwasilisha nyaraka zifuatazo;-
Kivuli cha Hatimiliki au Barua ya Toleo au Leseni ya Makazi
Kivuli cha kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA
Iwapo mmiliki ni Kampuni au Taasisi,vivuli vya hati ya usajili, taarifa za wanahisa,vitambulisho vya Taifa vya wanahisa.
Wamiliki watakaoshindwa kuwasilisha taarifa zao wenyewe kutokana na sababu mbalimbali wanaruhusiwa kuwasilisha taarifa hizo kupitia kwa wawakilishi wao ambao watawatambulisha kwa barua rasmi.
Limetolewa kwa ushirikiano wa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba na Makazi pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea
20 JULAI, 2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa