Tanzania ni miongoni mwa nchi 43 kati ya wanachama 55 za Umoja wa Afrika (AU) waliosaini na kuridhia Makubaliano ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) ambapo ilijiunga rasmi Januari 1, 2021.
TANTRADE imeundwa kwa sheria Na. 4 ya bunge ya mwaka 2009 kwa lengo la kusimamia majukumu ikiwemo na Kuwa kitovu cha hadhi ya kimataifa chenye nafasi kuu ya kuwezesha, kukuza na kusaidia biashara kwa ubora wa kiuchumi na Kutafuta fursa kwa makampuni ya Kitanzania, hasa Biashara Ndogo, Ndogo na za Kati (SMEs), na kuwaunganisha washirika wa kibiashara Duniani.
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara chini ya taasisi ya Tantrade inaratibu shughuli za utafutaji wa masoko ya bidhaa za Tanzania ndani na Nje ya Nchi kwa lengo la kukuza uchumi wa Nchi na kusaidia upatikatikanaji wa Masoko ya bidhaa kwa Wananchi.
Akizungumza Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Ruvuma Joel Mbewa alisema “Tanzania ni mwanachama rasmi wa AfCFTA toka 2021 ikiungana na nchi zingine ambazo ni Ghana, Kenya, Rwanda, Niger, Chad, Eswatini, Guinea, Cote d’lvoire, Mali, Namibia, South Africa, Congo, Rep, Djibouti, Mauritania, Uganda, Senegal, Togo, Egypt, Ethipia, Gambia, Sahrawi Arab Democratic Rep, Sierra leone , Zimbabwe, Burkina Faso,Sao Tome & Principe, Equatorial Guinea, Gabon, Mauritius.”
Hayo yamejiri leo tarehe 30 Agost 2023 katika mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea ambayo yamehudhuriwa na wafanyabiashara Mkoani Ruvuma yaliyotolewawa na TANTRADE kwa lengo la kutoa elimu juu ya kutumia fursa za matumizi ya Soko Huru za Afrika na fursa zilizopo .
Mbewa alisema, Fursa hizo zitawezesha kuboresha bidhaa wnazozalisha ili kukabiliana na soko shindani lililopo katika soko huru la Africa, kuongezeka kwa idadi ya namba za bidhaa zinazozalishwa ili kupata kufahamika, kupata wanunuzi wa malighafi zilizopo mashambani kwa kuwa kutakuwana soko la kutosha.
Kwa upande wake Afisa Biashara Mkuu TANTRADE Crispin Mathew Luanda alisema lengo kuu la mafunzo haya ni kuhamasisha wafanyabiashara Afrika waweze kutumia fursa zilizopo Afrika bila mashariti yoyote kwa lengo la kuongeza uchumi wa nchi na maisha ya jamii kwa ujumla.
Luanda alisema Tanzania ni moja ya Nchi ambazo zimeingia Mkataba wa Soko huru la Afrika kati ya nchi 8 ambazo zimepewa kipaumbele ikiwemo na Egypt, Rwanda, Morocco, Africa ya Kusini.
Kwa upande wa wafanyabiashara wakizungumza na chanzo hiki ambapo wametoa shukrani kwa upande wa Serikali kutoa mafunzo ya namna ya kutumia Soko huru la Afrika ambyo yatawezesha kufungua fursa na kuinua kipato cha Nchi, kuongeza uchumi kwa wafanyabiashara kwa ujumla.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa