Umoja wa Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania TAPSHA “ Tanzania Primary School Head Teachers Association ambao umesajiliwa na kutambulika kisheria ambapo uliundwa kwa lengo la kuwaunganisha walimu wakuu wote ngazi ya Halmashauri, Mkoa hadi ngazi ya Taifa.
TAPSHA Manispaa ya Songea ina jumla ya wanachama 92 kati yao shule 81 ni za Serikali na 11 ni shule binafsi ambapo kupitia umoja huo wameweza kufanikisha kutatua changamoto mbalimbali kwa kushirikiana na viongozi ngazi ya Halmshauri ambao umepelekea kufanya vizuri kitaifa na kuzawadiwa cheti cha pongezi kwa Afisa Elimu Manispaa ya Songea kwa malezi bora ya walimu hao.
Hayo yamejili katika kikao kazi cha mwaka kilichofanyika leo 21 juni 2023 katika ukumbi wa SACOS ya Walimu kilichohudhuriwa na viongozi kutoka Halmashauri, Wanachama na Wadau wa Elimu kwa lengo la kufanya tahimini na kuboresha Taaluma katika Manispaa ya Songea.
Akizungumza Afisa Elimu Manispaa ya Songea Frank Sichalwe “amewataka wakuu wa shule wote kuongeza uwajibikaji na kubaini changamoto za kitaaluma na namna ya kuzitafutia ufumbuzi ili kuleta mabadiliko chanya ya ufaulu kwa wanafunzi.” Alisisitiza
Naye Menyekiti wa TAPSHA Manispaa ya Songea Mwl. Siwetu Ahamadi amesema TAPSHA imejiwekea mikakati ambayo itawezesha kuinua hali ya ufaulu kwa wanafunzi ikiwemo na kuendelea kusimamia na kuandaa mitihani ya upimaji “pre-National kwa madarasa yenye mitihani ikiwemo na darasa la saba, na darasa la nne.
Kwa upunde wa Walimu wakuu waliohudhuria kikao hicho wamesema umoja huo unawasaidia katika kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi na kuwaweka karibu. “ wameshukuru”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa