NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA,
10.09.2021.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema leo tarehe 10 Septemba 2021 ameongoza kikao cha kufanya tathimini ya mbio maalumu za mwenge 2021 kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri 3 ambazo ni Halmashauri ya Manispaa Songea , Halmashauri ya Madaba na Halmashauri ya Wilaya ya Songea, kwa lengo la kujadili changamoto pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyojitokeza katika mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru 2021 Wilaya ya Songea.
Pamoja na changamoto mbalimbali zilizojitokeza Wilaya imejipanga kuhakikisha inasimamia miradi yote vizuri pamoja na kuahidi kufanya vizuri zaidi katika msimu ujao wa mbio maalumu za mwenge Taifa.
Mgema ametoa pongezi kwa wataalamu kwa kuweza kufanikisha na kuhitimisha kukimbiza mwenge ndani ya Wilaya ya Songea, na miradi yote iliyokaguliwa kuweza kupitishwa kwa kuweka mawe ya msingi, kufungua, kuzindua na kukaguliwa.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa