TATIZO la maji katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma litabakia kuwa historia baada ya serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa kutoa kiasi cha zaidi ya Dola milioni 50 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji katika kata zote 21 na mitaa yote 95 iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la madiwani la manispaa ya Songea,Mbunge wa Jimbo la Songea mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Damas Ndumbaro amesema mradi huo unatekelezwa na nchi ya India na kwamba mradi unatarajia kuanza Septemba 2019.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa