WAKALA wa Majengo Tanzania(TBA) wamekabidhi bweni mjoa katika shule ya sekondari ya wasichana Songea ambalo limekarabatiwa kwa zaidi ya shilingi milioni 102.
Kabla ya kukabidhi bweni hilo umefanyika ukaguzi wa bweni hilo la ghorofa likiwa uwezo wa kuchukua wanafunzi 110.
Ukaguzi umewashirikisha watalaam toka Manispaa ya Songea wakiwemo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Frowin Komba,Mhandisi wa Ujenzi Karoline Kandonga,Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Songea Tupoke Ngwala,Mwakilishi wa TBA Mhandisi Eugenics Thomas na viongozi wa serikali ya wanafunzi
Akizungumza baada ya kukabidhi mradi huo Mwakilishi wa TBA Mhandisi Eugenics Thomas amesema ukarabati wa bweni hilo ulianza Januari 10 mwaka huu na kwamba ukarabati wa mabweni mengine matano unaendelea kufanywa katika shule hiyo kwa awamu na kwamba ukarabati wa bweni la pili unaanza rasmi Aprili mwaka huu.
Ametoa rai kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ambao wataingia katika bweni hilo lenye vitanda 110 na makabati 110 kuhakikisha wanatunza bweni hilo kwa kuwa serikali imetumia fedha nyingi za kukarabati.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Songea Tupoke Ngwala amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya kufanyia ukarabati majengo yote ya shule hiyo yakiwemo mabweni na majengo ya utawala.
Shule ya sekondari ya wasichana Songea ni miongoni mwa shule kongwe nchini ina wanafunzi 874 wanaosoma kidato cha tano na sita ambayo ilianzishwa mwaka 1974.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari wa Manispaa ya Songea
Machi 23,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa