Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC) limeanzishwa kwa kifungu cha 40 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Na. 12 ya mwaka 2003 kama ilivyorekebishwa mwaka 2017 ikiwa na majukumu ya kuwa kiungo baina ya Watumiaji wa Huduma zinazosimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Watoa Huduma, TCRA na Serikali.
Baraza hilo linatekeleza Mpango mkakati wa miaka mitano 2019/2020-2025/2026 wenye lengo la kiuboresha ustawi wa watumiaji na kuongeza uelewa wa masuala ya huduma bidhaa za mawasiliano ni Dira ya Baraza ambalo ni chombo imara na cha kutegemewa katika kutetea haki na maslahi ya watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano pamoja na kuleta maelewano miongoni mwa wadau wa sekta ya Mawasiliano.
Hayo yamejili wakati wa semina ya kuelimisha na kuhamasisha Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano iliyoshirikisha makundi mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa, Wajasiliamali, Wanawake, Vijana, Mafundi Simu, Mawakala wa usajili laini za simu, wawakilishi wa NGO’S na viongozi wa dini kwa lengo la kuelimisha watumiaji, kushauriana na kupokea maoni uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea tarehe 31 Januari 2023.
Katibu Mtendaji Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano TCRA CCC Bi Mary Shao Msuya alisema jukumu la kutunza miundombinu ya Mawasiliano ni la wananchi ambao ni watumiaji na endapo utaona kuna dalili yoyote ya uhalifu unapaswa kutoa taarifa polisi kwa hatua zaidi.
Bi Msuya alisema Mkutano huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa majukumu ya baraza ambayo wamejipangia mwaka huu yenye kuelimisha, kuhamasisha, kupokea maoni kutoka kwa watumiaji na kuanzisha kamati katika Mkoa wa Ruvuma ambayo ni kamati ya 18 kati ya hizo kamati 16 ni za Tanzania Bara na kamati mbili ni za Tanzania Visiwani.
Aliongeza kuwa Sekta hiyo ina changamoto nyingi ikiwemo na uelewa mdogo kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano ikiwemo na kutumia simu zilizosajiliwa kwa jina la mtu mwingine na kutuma picha zisizo na maadili.
Akibainisha Wajibu wa Watumiaji wa huduma za Mawasiliano ni kutii sheria za nchi za matumizi halali ya huduma, kulipia huduma wanazozitumia, kuhifadhi mazingira na utunzaji wa mawasiliano, kuelewa huduma wanazopata, kuwa makini katika matumizi na kujilinda, kulalamika na kuwasilisha malalamiko kuhusiana na huduma na kutambua kasoro katika matumizi na utoaji wa taarifa.
Kwa upande wake Afisa kutoka sehemu inayoshughulikia masuala ya wateja na watumiaji TCRA Sohela Mabeyo alisema hadi Septemba 2022 Tanzania jumla ya laini za simu 58,118,961, ambapo kwa Mkoa wa Ruvuma hadi kufikia June 2022 jumla ya laini 1,510,498, hadi kufikia june 2022 jumla ya watumiaji wa Internet 31,122,163, pia hadi kufikia juni 2022 akaunti za PESA za mtandao ni 39,590,502.
Akibainisha makosa mbalimbali ya uvunjifu wa sheria ambayo ni pamoja na kupiga picha zilizokinyume na maadili, kufanya biashara ya utapeli mtandaoni, kupigiwa simu na matapeli ambapo alisema namba ya huduma kwa Wateja ni 100 pekee ambapo amewataka watumiaji kutumia mitandao kwa uangalifu ili kuepuka uvunjaji wa sheria. . “Alisisitiza.”
Alisema usipokee maelekezo kutoka namba yoyote isiyokuwa namba 100 kinyume na hapo wengi huishia kutapeliwa ambapo alitoa maelekezo kuwa ikitokea umetapeliwa kwa njia ya simu tafadhali tumia namba 15040 ambayo utaingia kwenye uwanja wa ujumbe (SMS) utaandika neno UTAPELI kwa herufi kubwa na kama kuna ujumbe utaweka kisha utatuma 15040 hatimaye hiyo namba itafungiwa. “Mabeyo alisisitiza.”
Kwa upande wa wadau waliohudhuria semina hiyo walitoa shukrani kwa Serikali kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yamewasaidia katika kutambua matumizi bora ya huduma za mawasiliano.
Mwisho
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI..
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa