PEMBE za tembo kutoka pori la Akiba la Liparamba Mkoani Ruvuma zimebainika kuongoza kwa uzito ukilinganisha na pembe za tembo kutoka hifadhi na mapori mengine ya wanayampori nchini.
Afisa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma Africanus Challe anasema pembe za tembo wa Liparamba zimebainika kuwa na uzito wa kilo karibu 140 kwa pembe moja ,wakati katika hali ya kawaida pembe za tembo zina uzito wa kilo 100 kwa pembe moja ya tembo .
Tembo ni mnyama wa pili kwa ukubwa duniani ambaye anakadiriwa kuwa na kilo 7000 sawa na tani saba.Wataalam wa wanyamapori wanasema tembo anaweza kuishi kati ya miaka 60 hadi 70,tembo jike hubeba mimba kwa miaka miwili,tembo mtoto huzaliwa na kilo kati ya 80 hadi 120,chakula cha tembo kwa siku ni kilo 300 na maji kwa siku tembo anakunywa lita 40.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Julai mosi,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa