Uongozi wa Wilaya ya Songea kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma imeendesha Tafrija ya Kumuaga aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Bi Pendo Daniel na kumkaribisha Katibu Tawala Mtela Mwampamba iliyofanyika katika ukumbi wa Herritage Cottage tarehe 08 Julai 2023.
Akisoma maudhui ya tafrija hiyo Mkurugenzi Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko alisema “Ndugu yetu DAS Pendo Daniel uliyekuwa Katibu Tawala Wilaya ya Songea, kama Mkoa bado tupo naye kwa kuwa Mbinga ni sehemu ya Mkoa wa Ruvuma pia ukikaa na wenzio katika kipindi kirefu akiondoka inasononesha na leo hii tunakupongeza kwa Uteuzi ulioupata hongera saana.”
Akitoa neno la shukrani Bi Pendo Daniel alisema “kwa mara ya kwanza aliteuliwa 2016 na hadi kufikia 2023 ameteuliwa tena na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo ametoa shukrani kwa kuteuliwa na kuaminiwa katika nafasi hiyo na kwenda kuwatumikia Wananchi wa Wilaya ya Mbinga, hivyo ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Viongozi wote, wadau pamoja na wananchi. “ ameshuku
Kwa Upande wake Mtela Mwampamba alisema “Tarehe 01 Julai 2016 aliteuliwa kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Kisarawe na alitumikia kwa muda wa miaka 4 minne ambapo kwa mwaka 2023 ameteuliwa kuwa DAS Songea, hivyo ameahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi na Vingozi, Alisisitiza”
Akizungumza Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Joel Mbewa kwa niaba ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa alisema “ Desturi ya kuwaaga watumishi wanaohama na kuhamia ni Desturi njema inayopaswa kuigwa, japokuwa sio kila Taasis inaweza kufanya hivyo, lakini mmelipa kipaumbele na kufanikisha kutekeleza jukumu hili hongereni sana.”
Mbewa aliongeza kuwa Utumishi sio kufanya kazi tu bila kuzingatia maisha na ustawi wa Mtumishi bali watumishi wanapaswa kujiwekea utamaduni wa kupanga kukutana kwa ajili ya kubadilishana mawazo, uzoefu, kama ilivyotendeka leo katika tukio la kumuaga na kumkaribisha mtumishi ambapo zoezi hilo linafanyika nje ya masaa ya kazi.
Mwisho alimtakia kazi njema Bi Pendo Daniel mahala aendako katika kituo chake kipya cha kazi Wilaya ya Mbinga na kumkaribisha Katibu Tawala Mtela Mwampamba katika Wilaya ya Songea.
Imeandaliwa na
Amina Pilly
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa