MBUNGE wa Songea mjini Dk Damas Ndumbaro anakusudia kufungua matawi ya soka ya Majimaji katika kata zote 21 za Manispaa ya songea ili kuhakikisha timu hiyo ambayo ni kioo cha mkoa wa Ruvuma inaendelea kuutangaza mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza Na wananchi wa kata ya Mjimwema katika Manispaa ya songea,DK.Ndumbaro amesema Timu ya Majimaji ni kiwanda kwa sababu uwepo wake umetoa ajira kwa wachezaji na viongozi na kwamba timu zinapofika kucheza kwenye uwanja wa Majimaji zinachangia kuongeza mapato ambayo yanabaki kwa wananchi wa mji wa songea.
Amesema utafiti umebaini kuwa katika msimu mmoja Timu ya Majimaji inaingiza zaidi ya shilingi bilioni moja ambazo zinatumika katika Manispaa ya Songea hali ambayo inaongeza mzunguko wa fedha na kuongeza mapato.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa