Timu ya wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Eng. Gilbert Simya wamefanya ziara ya kutembelea miradi 11 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 3,591,415,327 ambapo kati ya fedha hizo kiasi cha 2,530,493,527 ni fedha za Serikali kuu na Wafadhili na kiasi cha 1,060,921,800 ni fedha za mapato ya ndani ya Halmshauri.
Ziara hiyo imeanza leo tarehe 17 Novemba 2023 na kuhitimishwa mnamo tarehe 18 Novemba 2023 kwa lengo la kutembelea na kukagua mradi wa Ujenzi wa Hosptali ya Halmashauri unaojengwa kwa thamani ya Bil. 1 ambao umeanza kutoa huduma ya awali ya matibabu OPD, Ujenzi wa shule ya Chief Zulu Academy shule ya Mchepuo wa lugha ya kiingereza inayojengwa kwa thamani ya Mil. 500 fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.
Miradi mingine iliyotembelewa ni ujenzi wa shule ya Sekondari (mpya) ya Lawrence Gama iliyopo kata ya Msamala inayojengwa kwa thamani ya Mil. 500 fedha kutoka kwa SEQUIP, Ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa, mabweni 4, na vyoo matundu 15katika shule ya Emmanuel Nchimbi kwa thamani ya Mil 777.5 fedha kutoka Serikali kuu, Ukamilishaji wa Zahanati ya Makambi kwa thamani ya Mil. 50 pamoja na ukarabati wa vyumba 3 vya madarasa shule ya Msingi Matogoro kwa thamani ya Mil. 40.
Akitoa pongezi kwa kamati za ujenzi, Wataalamu wa Manispaa kwa usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ambapo ametoa wito kwa Manispaa ya Songea kuandaa walimu bora watakaoweza kusimamia na kufundisha wanafunzi katika shule ya Chief Zulu Academy.
IMEANDALIWA NA ;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa