Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ametoa pongezi kwa Wataalamu na Viongozi wa Manispaa ya Songea katika kufanikisha kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ni ujenzi wa vyumba vya madarasa 76 ambavyo vimekamilika.
Pololet alisema lengo kuu la kutembelea miradi hiyo ni kufanya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa 76, viti na madawati ili kujiridhisha na hatua iliyofikia kwa kila mradi kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023.
Alisema Wilaya ya Songea ilipokea fedha za kujenga madarasa 96, kati ya hayo madarasa 10 yamejengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea, madarasa 10 katika Halmashauri ya Madaba na madarasa 76 yamejengwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambayo ujenzi wake umekamilika. “ Pololet alipongeza”
Hayo yamejili katika ziara ya ukaguzi wa miradi iliyofanyika leo tarehe 19 Desemba ambayo iliongozwa na kiongozi huyo ambapo alitembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa 3 katika shule ya Sekondari Sili, ujenzi wa vyumba vya madarasa 6 katika shule ya Sekondari Luwawasi, ujenzi wa vyumba vya madarasa 6 shule ya Sekondari Lizaboni, madarasa 6 shule ya Sekondari Chandarua, madarasa 2 sule Sekondari Matogoro, madarasa 3 shule ya Sekondari Mashujaa pamoja na ujenzi wa madarasa 2 shule ya Sekondari Mateka.
Aliongeza kuwa Mafanikio yaliyopatikana yametokana na ushirikiano kati ya wataalamu na viongozi mbalimbali ambayo yamesaidia kuonesha taswira nzuri ya usimamizi imara wa miradi Mkoani Ruvuma.
Mhe. Pololet ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha shilingi Bil.3.2 kwa ajili ya kujenga madarasa 156 Mkoa wa Ruvuma kati ya hizo Manispaa ya Songea ilipokea kiasi cha fedha Bil. 1.52 ambazo zimetumika kujenga madarasa 76 ambayo ujenzi wake umekamilika. “Alishukuru.”
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa