MKUU wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema ametoa rai kwa vikundi vya wanawake ,vijana na wenye ulemavu ambao wamepewa mikopo kupitia Idara ya maendeleo ya Jamii katika Manispaa ya Songea kuhakikisha kuwa fedha hizo wanazitumia kujikwamua kiuchumi.
Mgema ameyasema hayo katika hafla ya kukabidhi mikopo kwa vikundi hivyo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.Mgema amesema mapato wanayo yakusanya kupitia vyanzo vyao vya ndani asilimia 10 ya mapato hayo yanakwenda kwa wananchi ambao ni wanawake, Vijana na wenye ulemavu kwa ajili ya kuweza kuendeleza biashara yao vizuriVile vile Mgema amewasihii sana wajasiriamali wakitaka faida kubwa inabidi wawe na mtaji mkubwa kwahiyo waache kulimbikiza malejesho ambayo ni kikwazo kikubwa katika kuongezeka kwa mkopo na pesa ikiwa nyingi wataweza kuacha na mikopo ya milioni 1 kwa kila kikundi
Kwa upande Naftari Saiyoloi Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Songea amesema kwa mwaka huu wa fedha 2019 wamejipanga kutoa kiasi cha shilingi milioni 124, lakini watakazo toa ni chini ya hizo kwa sababu fedha zinazo tokana na vyanzo vya ndani zaizi ya milioni 94, wanawake watapata Zaidi ya milioni 37, Vijana watapa Zaidi ya milioni 37, na watu wa makundi maalumu watapata Zaidi ya milioni18
amesema asilimia 10 ya fedha iliyo kusanywa robo ya mwaka wa fedha ya serikali julai mpaka semptemba 2019 wanazitoa leo mwezi octoba lakini wanazo milioni 30 zinazo tokana na malejesho zinaludi tena kwao ambayo ni marejesho ya waliyo chukuwa mwanzo wanapewa watu wengine katika mgao wa nne, nne na mbili kwa wanawake watapata milioni 12 vijana watapata milioni 12, na watu wa makundi maalumu watapata milioni sita
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa