Afisa Tarafa Magharibi Songea Mjini Dismas Komba amewataka wananchikumtumaini mungu katika imani nakujenga upendo kwa jamii ili kuondoa chuki, tama mbaya na visasi ambavyo huchochea kufanyika kwa vitendo vya ukatili.
Rai hiyo imetolewa tarehe 10 desemba 2024 siku ya kilele cha kampeni ya siku ya 16 ya kupinga ukatili ambayo imefanyika katika kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea.
Akzungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Songea, alisema “miongoni mwa kata zinazoongoza watoto chini ya miaka 18 kujishughulisha na kazi mbalimbali ni pamoja na kata ya Ruvuma, Majengo, Bombambili, na Lizaboni ambapo watoto hao huonekana wakifanya biashara katika soko la jioni.”
Amewataka wataalamu wa maendeleo ya jamii Manispaa ya Songea kufanya tafiti ili kubaini nini kinsababisha kuongezeka kwa ajira za watoto.
Akizungumza mratibu wa maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia Manispaa ya Songea Bi Joyce Mwanja alisema, Katikia kipindi cha kuanzia Juni 2023 hadi Septemba 2024 Halmashauri ya Manispaa ya Songea imepokea kesi za ukatili ikwemo na kesi ya Ukatili wa kingono (21) Wanawake 17 na Wanaume 4, Ukatili wa kimwili (20) wote ni Wanawake, Ukatili wa kisaikolojia (18) wote ni Wanawake, Ukatili wa kiuchumi kesi (04) Wanawake 03 na Wanaume 01
Aidha, licha ya idadi ya kesi za ukatili zilizotolewa taarifa, pia kuna jumla ya watoto waliotambuliwa katika utumikishwaji ambao idadi yao ni wasichana 25 na wavulana 29.
Aliongeza kuwa Lengo la kampeni hii ni kuongeza ushawishi, kubadilishana taarifa, uzoefu, kujenga uwezo wa pamoja, matumizi mazuri ya raslimali zinazopatikana na kuunganisha nguvu za asasi za kijamii katika kuhamasisha, kuelimisha, kukemea na kuchukua hatua kwa pamoja ili kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii.
Kaulimbiu ya mwaka 2024 ‘’Kuelekea miaka +30 ya Beijing Chagua Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia.’’
Kauli mbiu hii inalenga kupaza sauti ya pamoja na ili kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu athari hasi za ukatili wa kijinsia na njia za kuondokana na ukatili huo katika jamii.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa