Ukatili wa kijinsia ni kitendo ambacho kinafanywa na mtu kwa kumfanyia mtu mwingine bila kujali umri, maumbile, kabila, rangi, dini, lakini matukio mengi huwagusa wanawake na watoto kwa Kwakufanyiwa ukatili wa kimwili, kingono, kiuchumi na kisaikolojia.
Hayo yamebainika siku ya kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na watoto yalifanyika katika viwanja vya zimanimoto tarehe 10 disemba 2020 yaliyodhaminiwa na wadau kutoka USAID- Boresha afya kwa lengo la kukuza uelewa juu ya ukatili wa kijinsia kutoka ngazi ya chini ya jamii hadi ngazi ya Taifa.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala Wilaya Pendo Daniel ambaye alianza kwa kutembelea vibanda vya maonesho mbalimbali ikiwemo na Upimaji wa Virus Vya Ukimwi.
Pendo alisema “ ni lazima tutambue kuwa hiyo ni fursa ya pekee ambayo hutoa nafasi ya kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu haki za binadamu hususani haki za wanawake na watoto ambao hunyanyasika sana kutokana na unyonge walionao, na hatuna budi kuitumia fursa hiyo kwa ajili ya kuelimisha jamii, na kukemea vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia kama ukandamizaji wa wanawake na watoto”.
Serikali kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, Wazee na watoto ili kuandaa na kutekeleza Mpango huu wa watoto ( MTAKUWA 2017/2021) ukiwa umejidhatiti kusimamia mambo yote yanayohusu ulinzi wa mwanamke na mtoto.
Naye Afisa Ustawi wa jamii Manispaa ya Songea Devotha Ndunguru alisema” ukatili wa kijinsia unaweza kusababisha Migogoro ya ndoa, maambukizi ya VVU, ulemavu wa kudumu, upotevu wa maisha, mauaji ya watoto, mimba za utotoni, kuugua, na mauaji ya watoto wa mtaani.
Ili kuepukana na madhara yatokanayo na ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto ambapo alisema hatuna budi kuleta ushirikiano kwa wadau wote wakiwemo wadau wa Afya, polisi, ustawi wa jamii, maendeleo ya jamii, mahakama, pamoja na jamii kwa ujumla ili kutokomeza vitendo vinavyosababisha ukatili wa kijinsia. “Devotha alibainisha”.
Alisema mwaka 2019/2020 mashauri ya watu waliofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia me 439, ke 469 kati ya hizo kesi zilizopo mahakamani 236, na zilizoshinda kesi 36.
Amezitaja Sababu ambazo husababisha ukatili wa kijinsia ni pamoja na uelewa mdogo wa wananchi juu ya ukatili wa kijinsia, Umaskini, ukosefu wa elimu, ulevi, wivu wakimapenzi, mapungufu katika sheria pamoja na sababu za kiuchumi.
Alitabanaisha kuwa wahanga wa ukatili wa kijinsia walio wengi hawaripoti matukio kwasababu ya mila potofu, uelewa duni, umaskini, na kukosekana kwa vyombo vya kushughulikia ukatili ngazi ya jamii.
Aidha katika kukabiliana na changamoto hizo, Manispaa ya Songea imejiwekea mikakati ya kudhibiti matukio ya ukatili wa kijinsia kama kuimarisha mfumo wa utoaji huduma kwa wahanga, kuimarisha kamati za ulinzi wa mwanamke na mtoto, na kuendelea kutekeleza mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ( MTAKUWA).
kauli mbiu; TUPINGE UKATILI WA KIJINSIA MABADILIKO YANAANZA NA MIMI.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA .
11 disemba 2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa