KILA mwaka inapofika Juni 5 ni siku ya mazingira duniani wa mazingira ya ardhini,hewani na majini ambao unaendelea kufanyika kwa kasi kubwa kila siku unaiweka Dunia njia panda.
Wataalam wa mazingira wanasema hali hiyo isipodhibitiwa yatatokea maangamizi kwa viumbehai waliopo katika Sayari ya Dunia wakiwemo binadamu, wanyama, mimea, ndege,wadudu na viumbe hai wengine.
Athari za uharibifu na uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu kama uchimbaji wa madini, kuharibu vyanzo vya maji,uchomaji na ukataji miti hovyo,Moshi wa viwandani,matumizi ya kemikali za sumu na shughuli nyingine za uchafuzi.
Uchafuzi na uharibifu wa mazingira ardhini,majini na nchi kavu umekithiri katika kiwango ambacho kinatishia kutoweka kwa sayari ya Dunia na viumbehai, endapo hatua za makusudi hazitachukuliwa kuinusuru hali hiyo.
Kasi ya kutoweka kwa maji inaongezeka,tatizo la upatikanaji wa maji pia linaongezeka kutokana na kuongezeka kwa ukame unaosababishwa na shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji.Vita ya kugombania maji inakuja.
Wanasayansi wanasema shughuli mbalimbali za kibinadamu zimesababisha kuongezeka kwa joto la Dunia kwa nyuzi 0.85 na kusababisha madhara yote yanayotokea hivi sasa duniani yakiwemo ukame,magonjwa,mafuriko na mabadiliko ya tabianchi.
Hata hivyo wanasayansi wanatahadharisha kuwa iwapo joto duniani litaongezeka hadi kufikia nyuzi joto 1.5 ambalo ni ongezeko la nyuzi joto 0.65 viumbehai wote waliopo duniani hawataweza kumudu kuishi.
Kwa mujibu wa wanasayansi Mwaka 2012 ongezeko la joto duniani lilikuwa nyuzi 0.7 na kwamba kiwango cha joto kilifikia nyuzi 0.85 hadi kufikia mwaka 2015.
Hata hivyo watalaam wanaitaja njia pekee ambayo inaweza kuinusuru dunia katika janga la mabadiliko ya tabianchi ni kupanda miti ya kutosha kila mwaka na kupambana na watu wote wanaokata miti hovyo na kuharibu mazingira kwa ujumla wake.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO zinaonesha kuwa zaidi ya watu bilioni mbili kutoka nchi zaidi ya 40 zenye mabonde ya mito wapo katika vita ya kugombania maji kutokana na uchafuzi wa vyanzo vya maji unaoendelea kwa kasi duniani kote na kusababisha maji kukauka.
Utafiti mpya umeonesha kuwa watu milioni sita kote duniani wanakufa kila mwaka kutokana uchafuzi wa mazingira ya hewa ambapo asilimia 90 ya watu wote duniani wanavuta hewa chafu.
Mazingira salama ndiyo msingi wa uhai wetu,mazingira yakiwa na afya tutakuwa na afya,mazingira yakiugua tutaugua na mazingira yakifa viumbe wote tunafutika katika uso wa dunia.
Mwandishi wa Makala haya ni Afisa Habari wa Manispaa ya Songea
Baruapepe albano.midelo@gmail.com,simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa