Tutakipandisha hadhi kituo cha Afya Mjimwema kuwa Hospitali
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk.Hamisi Kigwangalla amewahakikishia wananchi wa Manispaa ya Songea kuwa Kituo cha Afya Mjimwema kilichopo katika Manispaa hiyo kitapandishwa hadhi kuwa hospitali ya Wilaya.
Dk.Kigwangalla ametoa ahadi hiyo kabla ya kuzindua mradi wa uchunguzi wa saratani za mlango wa kizazi,matiti na magonjwa yasiyoambukiza katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Amesema kituo hicho cha Afya kimechelewa kupandishwa hadhi kuwa hospitali kutokana na kukosa vitengo muhimu ikiwemo chumba cha upasuaji ambapo hivi sasa tayari kituo hicho kina jengo la upasuaji,vifaa na watalaamu na kwamba huduma ya upasuaji imeanza kutolewa.
“Leo nimefarijika sana baada ya huduma za upasuaji wa dharura na huduma za kumtoa mtoto tumboni zinafanyika katika kituo cha Afya Mjimwema’’,anasema Dk.Kigwangalla.
Amesema wakati ukifika serikali itakipandisha hadhi kituo cha Afya Mjimwema kuwa hospitali ya wilaya na kwamba imedhamiria vituo vyote vya Afya 484 vilivyopo hapa nchini vitoe huduma ya upasuaji kama livyo katika kituo cha Afya Mjimwema.
Kituo cha Afya Mjimwema kilianzishwa Aprili 8,2002,Kituo hicho kina majengo nane yakiwemo Jengo la wagonjwa wa nje,Wodi ya Watoto na Wanawake,Wodi ya Wazazi na huduma za kujifungua, jengo la kutolea huduma za afya ya uzazi na mtoto na wodi ya Wanaume, jengo la Utawala, jengo la kuhifadhia maiti, nyumba mbili za watumishi na jengo la upasuaji.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa