• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

UFAHAMU MRADI WA BOOST KUJENGA MADARASA 12000 YA AWALI NA SHULE ZA MSINGI 3000

Tarehe ya kuwekwa: December 19th, 2022

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Vicent  Kayombo amewataka wataalam  kusimamia miradi kwa weredi ili  iweze kujengwa kwa ubora na viwango vinavyotakiwa.

Alisema Serikali imeweka utaratibu wa kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo  wataalamu ngazi ya Halmashauri na Mkoa  kwa lengo la kuimarisha   usimamizi wa miradi ya Serikali ili kufanikisha lengo tarajiwa.

Hayo yamejili katika mafunzo ya wataalamu zaidi ya 280  kutoka Mkoa wa Iringa, Njombe, na Ruvuma yaliyotolewa na Ofisi ya Rais  TAMISEMI  kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia kupitia mradi wa BOOST yaliyofanyika kuanzia tarehe  16-17/2022 katika kanda 9 katika Mkoa wa Iringa.



Akizungumza na washiriki wa mafunzo  elekezi  kwa timu za utekelezaji wa mradi wa BOOST kutoka kwenye Halmashauri na Mikoa alisema lengo kuu  mahususi la mafunzo haya ni pamoja na kuzijengea uelewa timu za utekelezaji  kuhusu mradi wa BOOST ambao utazingatia usimamizi wa fedha na manunuzi ya umma, kuandaa mpango wa utekelezaji wa boost, afua zitakazotekelezwa  kupitia mradi wa boost.

Mradi huo  wenye thamani ya takribani Trioni 1.15 sawa na Dola za kimarekani Milion 500 ambapo kati ya hizo Dola za Kimarekani 480, ni programu na Dola za Kimarekani Milioni 20 ni gharama ya uwekezaji wa mradi.

Mradi huo utafanyika kwa muda wa miaka 5 kuanzia 2021/2022 hadi 2025/26  ambapo utatekelezwa kwa awamu tofauti ambayo itajengwa madarasa 12,000 ya awali na shule za msingi 3000 kwa mwaka, kununua vifaa vya TEHAMA kwa shule  zaidi ya 800 za msingi  na vituo vya walimu kwa ajili ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji na mafunzo endelevu ya walimu kazini.  

Mradi huo utasaidia kuongezeka kwa uandikishaji  wa Elimu ya awali kutoka asilimia 76.9% kwa mwaka 2021 hadi asilimia 85% pamoja na kutekeleza mafunzo ya walimu kazini (MEWAKA) katika ngazi ya vituo vya walimu.

Miongoni mwa washiriki katika mafunzo hayo ni Afisa elimu kutoka kila Halmashauri na Mkoa, Afisa manunuzi, Afisa mipango, Afisa maendeleo ya jamii, Mhandisi, Mdhibiti ubora, Mratibu wa mradi, Katibu wa TSC Wilaya, Mhasibu, Mwalimu mkuu kutoka kila Halmshauri, na Afisa Habari kutoka ngazi ya Mkoa na Halmashauri.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii TAMISEMI Hilda Mgomapayo  alisema utekelezaji wa afua hiyo ni mpango salama kwa Elimu ya awali na  msingi  ambao unalenga kupunguza vikwazo vya upatikanaji wa elimu kwa watoto wote na waliopo katika mazingira hatarishi wakiwemo na wenye mahitaji maalumu pamoja na kuwezesha kukamilika mzunguko wa Elimu.

Mgomapayo alisema katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza mpango wa shule salama unalenga kuzifikia shule 6000 hadi kufikia 2026 kwa lengo mahususi la kuweka mazingira ya mapito salama kwa wanafunzi wanapokwenda shule na kurudi nyumbani. “alibainisha”

IMEANDALIWA NA;

AMINA PILLY;

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.

  




Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa