KISUKARI ni ugonjwa sugu ambao unatokana na sukari kuwa juu kwa muda mrefu kwenye damu.Kutokana na tatizo hilo kuwa tishio Shirika la Afya Duniani limeweka Novemba 14 kila mwaka kuadhimisha siku ya kisukari.
Kwa mujibu wa Geofrey Mdede Daktari wa Magonjwa ya Kisukari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma,kuna aina mbili za kisukari, ambapo aina ya kwanza huitwa Diabetes Type 1, na aina ya pili huitwa Diabetes Type 2.
“Diabetes Type 1 mtu anakuwa amezaliwa na kongosho ambalo halina uwezo wa kutoa kiasi cha kutosha cha kichocheo cha insulin. Wagonjwa wa aina hii, kwa kawaida huitaji kuwa wanachoma sindano za vichocheo vya insulin katika maisha yao yote”,anasema Dk.Mdede.Hata hivyo anabainisha zaidi kuwa katika aina hiyo ya kwanza ya ugonjwa wa kisukari, wagonjwa hugundulika mapema wakati wa utoto, au wakati wa ukuaji.
Kuhusu aina ya pili yaani diabetes type 2, Dk.Mdede anasema ugonjwa huo huwapata watu kuanzia umri wa miaka 45 na kwamba aina hii ya kisukari husababishwa na aina ya maisha ambayo watu wanaishi na aina ya vyakula vinavyotumika.Licha ya kwamba tatizo la ugonjwa wa kisukari ni la kidunia,Katika Mkoa wa Ruvuma ugonjwa wa kisukari ni tatizo kubwa hali ambayo inaleta athari kubwa kijamii na kiuchumi.
Daktari wa Magonjwa ya Moyo na Kisukari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma Dk.Mdede anasema hadi sasa wamesajiri wagonjwa 500 wa kisukari ambao wanapata matibabu bure.
Anazitaja dalili kuu za mtu mwenye kisukari kuwa ni kunywa maji sana,kupata kiu mara kwa mara,kuwa na njaa mara kwa mara na kukojoa mara nyingi.Takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO) zinaonesha kuwa hadi kufikia mwaka 2016 kuna watu milioni 422 duniani wanaougua ugonjwa wa kisukari.
Mwandishi wa makala haya ni Albano Midelo
mawasiliano albano.midelo@gmail.com,simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa