MKUU wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Pololet Mgema amewatahadharisha wananchi ambao kwa makusudi hawataki kujitokeza katika zoezi linaloendelea katika wilaya ya Songea la kujiandikisha kupata vitambulisho vya uraia.
Amesema Kukosa kitambulisho cha uraia ni kujiweka katika hatari ya kuitwa sio raia wa Tanzania .Zoezi la kuandikisha vitambulisho vya uraia katika wilaya ya Songea limeanza tangu Januari 3 mwaka huu ambapo hadi sasa zaidi ya watu 13,770 wameandikishwa.
Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya amesema bado kuna idadi kubwa ya watu ambao bado hawajaandikishwa.Kitambulisho cha Uraia ndiyo kitambulisho namba moja Tanzania,vitambulisho vingine vinafuatia.
Mkuu wa wilaya alikuwa anazungumza katika Mkutano wa dharura wa Baraza la madiwani la Manispaa ya Songea ,uliofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Alhaj Abdul Hassan Mshaweji.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa