HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imekuwa ikipokea dawa na vifaa tiba toka serikali kuu kila mwaka na dawa hizo hupelekwa moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma na wasambazaji yaani MSD.Hadi sasa hali ya upatikanaji dawa muhimu katika vituo vyetu vya kutolea huduma ni asilimia 91.1 hivyo ni ya kuridhisha.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Tina Sekambo amesema Halmashauri hununua dawa za nyongeza kufidia zile zinazokosekana MSD kupitia vyanzo vingine vya fedha ikiwemo Mfuko wa pamoja wa afya, Bima ya Afya, CHF na fedha za papo kwa papo zenye jumla ya Tshs. 83,978,000.00 kwa mwaka 2017/2018 na Tshs. 24,569,900.00 hadi kufikia Disemba 2018/2019.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa