UCHAFU sio tu unasababisha maradhi lakini pia unasababisha baadhi ya wanaume kukimbia nyumba zao na kutafuta wanawake wasafi.
Diwani wa Kata ya Mfaranyaki Manispaa ya Songea Seneth Yatembo akizungumza katika Jumamosi ya mwisho wa mwezi Januari ya usafi wa Mazingira,amewaasa akinamama ambao ndiyo nguzo ya familia kuhakikisha suala la usafi wa Mazingira,mwili na roho linakuwa endelevu.
Usafi wa Mazingira katika Manispaa ya Songea mwezi huu umefanyika katika Ghuba la Mbao Mfaranyaki ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema ambaye amewakilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Naftari Saiyoloi.
Akizungumza na wananchi wa Mfaranyaki Saiyoloi amesisitiza kuwa usafi ni gharama na kwamba kila mmoja anatakiwa kushiriki kikamilifu kufanya usafi ili kuepukana na magonjwa ambayo yanasababishwa na uchafu.
Kupitia siku hiyo maalum ambayo inafanyika mara moja kila mwezi,Kaimu Mkurugenzi huyo amewakumbusha wananchi hao kuchangia shilingi 2000 kila mwezi kwa kila kaya na kwa wafanyabiashara shilingi 4000 ambazo zimepitishwa katika mitaa ya Manispaa kuchangia usafi wa Mazingira.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa