SHIRIKA lisilo la kiserikali la USAID PROTECT limetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi shilingi milioni 46 katika chuo cha mafunzo ya Uhifadhi wa maliasili (CBCTC) kilichopo Likuyu wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.Vifaa hivyo vimekabidhiwa na Mwakilishi wa USAID Thadeus Binamungu kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Generali Gaudence Milanzi.Vifaa vilivyokabidhiwa ni jenereta moja,vionambali 10,GPS 10,Kompyuta mpakato tano,powerpoint mbili, na vitabu 40 kwa ajili ya kozi ya waongoza watalii.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha CBCTC Jane Nyau amelishukuru Shirika la USAID PROTECT kwa misaada ya vifaa mbalimbali ambavyo vimetolewa kwa chuo hicho ambayo imelenga kuboresha shughuli za utoaji mafunzo chuoni hapo hivyo kupunguza baadhi ya changamoto za muda mrefu ambazo zimekuwa zinakikabili chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 1995.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Generali Gaudence Milanzi amelishukuru shirika hilo kwa msaada huo ambao awali vifaa hivyo vilipangwa kukabidhiwa makao makuu ya Wizara hiyo jijini Dodoma na ameahidi serikali kuendelea kushirikiana na mashirika ambayo yanatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi kama linavyofanya Shirika la USAID PROTECT.
Imeandikwa na Albano Midelo
Mawasiliano albano.midelo@gmail.com,simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa