HAPA ni Kijiji Utamaduni cha Lesedi kilichopo nchini Afrika ya Kusini.Wakazi wa eneo hilo wametajirika kutokana na utalii wa kiutamaduni ambako kila siku wanapokea mamia ya watalii kutoka nchi mbalimbali duniani.Hakuna cha pekee hapa zaidi ya kupata maelezo kuhusu utamaduni wa makabila ya South Afica,vyakula vyao vya asili,nyumba zao,ngoma zao mila na desturi zao,hawa jamaa wanatengeneza fedha nyingi sana.
Mkoa wa Ruvuma una fursa kubwa ya kujiingizia fedha kwa kutumia Utalii wa kiutamaduni kwa sababu kuna makabila mengi yenye ngoma,vyakula vya asili,vinyago,nyumba za asili,mila na desturi kwanini nasisi tusianzishe RUVUMA CULTURAL VILLAGE?
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa michache nchini ambayo imebarikiwa na Mwenyezi Mungu kuwa na vivutio vya aina zote za utalii,ambazo ni utalii wa ikolojia na utamaduni.
Ruvuma na mapori manne ya wanyamapori ambayo ni sehemu ya mfumo wa Selous.Mapori hayo ni Selous lenye ukubwa wa kilometa za mraba 50,000,Pori la Liparamba lenye kilometa za mraba 571,Gesimasoa lenye kilometa za mraba 764 na Litumbandyosi lenye kilometa za mraba 464.
Hata hivyo utafiti umebaini bado kuna vivutio vingi ambavyo havijaibuliwa na kutambuliwa ili kutoa fursa za uwekezaji kwa watalii toka ndani na nje ya nchi.
Afisa Maliasili wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anasema vivutio hivyo vikiendelezwa vinaweza kuchangia pato la Taifa na kuinua uchumi wa wananchi na kwamba kinachotakiwa ni kuboresha miundombinu ya barabara na hoteli za kitalii ili kuvutia watalii kuvifikia vivutio hivyo.
Utafiti umebaini karibu kila wilaya iliyopo katika mkoa wa Ruvuma ina vivutio mbalimbali vya utalii vinavyoweza kufungua milango ya utalii katika wilaya husika na kutoa ajira kwa vijana kupitia sekta hiyo adimu hapa nchini na duniani kote.
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa michache nchini ambayo imebarikiwa na Mwenyezi Mungu kuwa na vivutio vya aina zote za utalii,ambazo ni utalii wa ikolojia na utamaduni.
Mkoa wa Ruvuma una mapori manne ya wanyamapori ambayo ni sehemu ya mfumo wa Selous.Mapori hayo ni Selous lenye ukubwa wa kilometa za mraba 50,000,Pori la Liparamba lenye kilometa za mraba 571,Gesimasoa lenye kilometa za mraba 764 na Litumbandyosi lenye kilometa za mraba 464.
Hata hivyo utafiti umebaini bado kuna vivutio vingi ambavyo havijaibuliwa na kutambuliwa ili kutoa fursa za uwekezaji kwa watalii toka ndani na nje ya nchi.
Afisa Maliasili wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anasema vivutio hivyo vikiendelezwa vinaweza kuchangia pato la Taifa na kuinua uchumi wa wananchi na kwamba kinachotakiwa ni kuboresha miundombinu ya barabara na hoteli za kitalii ili kuvutia watalii kuvifikia vivutio hivyo.
Utafiti umebaini karibu kila wilaya iliyopo katika mkoa wa Ruvuma ina vivutio mbalimbali vya utalii vinavyoweza kufungua milango ya utalii katika wilaya husika na kutoa ajira kwa vijana kupitia sekta hiyo adimu hapa nchini na duniani kote.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Serikalini
Mawasiliano yake albano.midelo@gmail.com,simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa