Manispaa ya Songea inaendelea na utekelezaji wa kupambana na utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano 5 kwa kutoa unasihi wa uandaaji wa chakula na ulaji unaofaa kwa akinamama wajawazito, wanaonyonyesha, walezi wa watoto wenye umri chini ya miaka 5.
Katika kukabiliana na utapiamlo Manispaa ya Songea imewekwa mikakati ambayo inasaidia kuondoa utapiamlo ambayo ni pamoja na kuhakikisha vyakula vyote vinavyopelekwa shule vinaongezwa viini lishe, kuhamasisha wazazi kuchangia chakula shuleni, kutoa lishe kwa VVU, na kutenga bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa lishe.
Mikakati hiyo imetamkwa kwa katika kikao cha kamati ya lishe cha robo ya kwanza kilichofanyika tarehe 04 Oktoba 2022 chenye lengo ya kutoa taarifa ya utekelezaji wa lishe kuanzia mwezi julai hadi Septemba 2022.
Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Songea Martin Mtani akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea amewasisitiza wazabuni wanaopeleka chakula mashuleni kuhakikisha wanapeleka vyakula vilivyoongezewa viini lishe kama unga, mafuta, na chumvi ili kujenga afya bora kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Mganga mkuu Manispaa ya Songea Amos Mwenda amesema jumla ya watoto chini ya miaka mitano 32,283 walinchunguzwa na kati yao 37,818 sawa na asilimia 0.117% ambapo kati yao 12 waligundulika kuwa na utapiamlo mkali ni asilimia 0.0003%, pia watoto 27 sawa na asilimia 0.07% waliochunguzwa na waligundulika kuwa na utapiamlo wa kadiri, na watoto 37,779 waliochunguzwa sawa na asilimia 99.8% hawakuwa na utapiamlo.
Afisa mifugo Manispaa ya Songea Rozina Chuwa alisema ili kukabiliana na utapiamlo idara ya mifugo imehamasisha wananchi na kufanikiwa kuunda vikundi 21 vya ufugaji wang’ombe wa maziwa ambavyo vinawezesha upatikanaji wa mazao ya maziwa.
Aliongeza kuwa Manispaa ya Songea imeweka malengo ya kuweka kituo cha kukusanyia maziwa ambapo itasaidia kuwa na uhakikia wa soko la maziwa, kutoa mwelekeo wa aina ya bidhaa itakayozalishwa na wasindikaji mtindi, siagi, samuli, kujenga makuzi bora kwa watoto pamoja na kufanya upimaji wa maziwa kabla hayajakwenda kwa mlaji.
Naye Afisa Lishe Manispaa ya Songea Albert C. Simkamba ametoa rai kwa Wahudumu wa afya na Watendaji wa kata na mitaa kuendelea kushirikiana kutoa elimu ya lishe kwa jamii kwa kutumia mikutano na vikao mbalimbali vya jamii na kuhamasisha utoaji wa lishe kwa watoto chini ya miaka mitano 5.
AMINA PILLY
MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa