WILAYA ya Songea mkoani Ruvuma imeweka mpango kabambe wa kutekeleza agizo la marufuku ya kutumia mifuko ya plastiki kuanzia Juni mosi 2019.Ili kuhakikisha agizo hilo linafanyiwa kazi kwa ufanisi mkubwa imeundwa Kamati ya kuhakikisha kuwa wilaya ya Songea inatekeleza mpango huo kwa asilimia 100.Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Pendo Ndumbaro ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ameitaja ratiba ya utekelezaji wa katazo hilo inaanzia Juni 3 hadi 14,2019 ambapo ametoa rai kwa wananchi wa wilaya ya Songea kushirikiana na watendaji wa serikali kuhakikisha mifuko yote ya plastiki inaondolewa na hakuna mwananchi yeyote ambaye ataendelea kuitumia kuanzia Juni Mosi mwaka huu kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai ambapo mtuhumiwa atafikishwa mahakamani na kupata adhabu ya faini au kifungo au adhabu zote mbili.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa