TANGU kuanzishwa kwa safari za anga za ATCL katika mkoa wa Ruvuma kwa kutumia uwanja wa ndege wa Songea kumeongeza fursa za kiuchumi katika mji wa Songea na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Ni vema wakazi wa mkoa wa Ruvuma kutumia fursa hii katika shughuli za utalii,leo mkoa wetu umefunguka,unaweza kufika Ruvuma kwa barabara ya lami toka Dar es salaam kupitia Lindi na Njombe na sasa unaweza kufika Ruvuma kwa njia ya anga ndani ya saa moja upo Ruvuma.
Kabla ya kuzinduliwa kwa safari za anga la ATCL, watalii walikuwa wanashindwa kutembelea vivutio adimu kama fukwe za ziwa Nyasa kwa sababu hawawezi kusafiri kilometa 1000 kwa barabara hivyo watalii walikuwa wanakwenda maeneo mengine ambapo sasa wameanza kufika Ruvuma ndani ya muda mfupi kuona vivutio mbalimbali vya utalii.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba anasema milango ya utalii Mwambao mwa ziwa Nyasa tayari imeanza kufunguka ambapo hivi sasa watalii kutoka nchi mbalimbali ikiwemo barani Ulaya wanafika kutembelea wilaya hiyo yenye vivutio adimu vya utalii.
Uwanja wa ndege wa Songea ni miongoni mwa viwanja 13 bora vya ndege Tanzania kati ya viwanja karibu 50 vilivyopo nchini.Uwanja huo ambao ulijengwa kati ya mwaka 1974 hadi 1980 umewekewa lami hivyo kuwa na uwezo wa kutua ndege majira yote masika na kiangazi.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Ruvuma
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa