Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas amewataka viongozi Mkoani Ruvuma kuwashirikisha Wananchi/Wazazi kwa kufanya Mikutano mbalimbali na kuona namna bora ya kutekeleza program jumuishi ya Taifa ya Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ili kuepuka matendo ya ukatili mwingi unaotokea nyumbani ukihusishwa na wadada wa kazi.
Hayo yamejiri leo 29 Septemba 2023 wakati wa uzinduzi wa program jumuishi ya Taifa yam malezi na maendeleo ya awali ya mtoto (PJT-MMMAM- 2021/2022-2025/2026) iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea iliyohudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, watumishi idara ya Maendeleo ya jamii pamoja na Viongozi kutoka TAMISEMI.
Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa amewataka “ Wakuu wa Wilaya kwenda kuzindua Program hiyo kiwilaya kabla ya mwezi wa 12.2023 ili Halmashauri iweze kufanya utekelezaji kadiri ya Mipango kazi yao pamoja na Wakurugenzi kuhakikisha wanafikisha program hiyo kwenye ngazi ya Kata,Vijiji na Mitaa ili kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa urahisi.” Alisisitiza”
Alisema Pamoja na mipango kazi yao ya Mwaka watakayo kuwa nayo ni Vyema pia kama Mkoa ushirikiane katika Kuihamasisha jamii kuwa na malezi yenye maadili, Lishe bora, kuhudhuria Kliniki mara tu mama anapokuwa mjamzito, Jamii nzima kuwa ni Walinzi Watoto lakini hili linzie ngazi ya familia, Kuhamasisha Wazazi kushiriki kwenye Maendeleo ya Elimu hususani ujenzi wa miundombinu ya Shule, kutengeneza Vifaa vya kujifunzia ambavyo vinapatikana kwenye jamii husika.
Mikakati mingine ni Wadau kuendelea kuisaidia Serikali katika kuchangia maendeleo ya ujenzi wa miundombinu rafiki kama vile madarasa changamshi ya Watoto wa Elimu ya Awali na Vituo vya kulelea Watoto Wakati wa Mchana.
Aidha, Lengo la kikao hicho ni kukumbushana na kuelekezana umuhimu wa kuwekeza kwenye umri wa miaka 0 - 8 kwani ndio umri wa ukuaji na ujifunzaji wa Mtoto huenda kwa kasi Zaidi.
Alibanisha kuwa, Program hii imekuja kuunganisha nguvu za pamoja kupitia Idara mbalimbali katika utekelezaji wa Mipango ya Serikali na Ilani ya Chama cha Mapiduzi inayomlenga Mtoto mwenye umri kuanzia miaka 0-8 ambapo kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 idadi ya Watoto walio na umri kuanzia mwaka 0 – 8 wapo 458,796 ikiwa ni asilimia 24.8 ya watu wote waliopo Mkoa wa Ruvuma.
Imeandaliwa na;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa