VIJANA watano katika Kata ya Matogoro Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wameanzisha kiwanda cha kutengeneza stick za kuchomea mishikaki na kuchokonolea meno.
Mbunge wa Songea Mjini Dkt.Damas Ndumbaro ametembelea kikundi hicho kinachoitwa Matogoro Stick Industry.
Akitoa taarifa ya kiwanda hicho,Katibu wa kiwanda hicho Suleiman Twaibu ameyataja malengo ya kuanzisha kiwanda hicho ni kuweza kutumia mianzi inayopatika kwa wingi katika Wilaya ya Songea na maeneo ya jirani ili kuzalisha bidhaa aina ya stick za kuchomea mishikaki na za kuchokonolea meno kwa afya ya watumiaji.
“Tumefanikiwa kutengeneza pesa kiasi cha shilingi milioni nne kupitia stick Industry,tumeweza kuboresha jengo la kiwanda kwa kuingiza umeme na kulipia madeni ya nyuma ya jengo hili’’,alisema Twaibu.
Alisema wametengeneza mashine nne za kuzalishia bidhaa zetu. Mashine ya kuchana mianzi,mashine ya kuchonga umbo na ukumbwa wa stick,Mashine ya kungarisha na mashine ya kufungasha bidhaa.
Katibu huyo amezitaja changamoto wanazopata katika kiwanda chao kuwa ni ukosefu wa eneo la kutumia katika utendeaji wa kazi zao,jengo wanalotumia hivi sasa ni jengo la CCM, hivyo wanatumia chumba kimoja wakati kazi yao inahitaji vyumba sita.
Amezitaja changamoto kuwa ni ukosefu wa mashine za kisasa zenye ubora wa kuzalisha bidhaa bora na kwa wingi,upatikanaji wa malighafi umekuwa changamoto baada ya wakulima wa zao hilo kupandisha bei,vifungashio pia bado ni changamoto ukilinganisha na ushindani katika soko.
Twaibu ameyataja matarajio ya kikundi hicho kuwa ni , kununua eneo la kutosha na kujenga miundo mbinu ya kiwanda katika maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za viwanda na kununua e shamba kubwa la zao la mianzi na kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha kilimo cha zao la miazi ili kiwanda hicho kipate malighafi za kutosha siku za usoni.
Imeandaliwa na Farida Mussa
Kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Julai 15,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa