IDARA ya Afya katika Manispaa ya songea kwa kushirikiana na wataalam wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamefanya operesheni katika maduka ya vipodozi mjini Songea na kufanikiwa kukamata aina mbalimbali za vipodozi ambavyo vinadaiwa kuwa na viambata vya sumu.
Hata hivyo Afisa Afya na Mratibu wa TFDA Manispaa ya Songea Vitalis Mkomela amesema uchunguzi wa vipodozi hivyo unaendelea kufanywa ambapo taarifa kamili ya aina za vipodozi vilivyokamatwa ,madhara yake kiafya na thamani ya vipodozi hivyo itatolewa baada ya sikukuu ya Jumatatu ya Pasaka.
“Uchunguzi wa awali umebaini vipodozi vilivyokamatwa vina viambata vyenye sumu ambavyo vinaweza kusababisha matatizo ya kiafya kwa watumiaji “,anasisitiza Mkomela.
Mkomela anavitaja viambata vyenye sumu vilivyopigwa marufuku kuwa Vingi vikiwa katika lugha ya kiingereza kuwa ni vyenye Chloroquinone (Hydroquinone na kemikali zingine),Steroids,Betamethasone,Beclomethasone, Hydrocortisone,Clobetasol,na Dexamethasone.
Viambata vingine anavitaja kuwa ni vyenye Mercury (Zebaki) na kemikali zinazotokana nayo Chloroform,Bithionol,Hexachlorophene,Mercury (Zebaki) ,Vinylchloride,Zirconium,kemikali zinazotokana Methyelene chloride,Halogenated salicylanilides, (Dimetabromsalan, Trimetabromsalan, na Chlorofluorocarbons Kwenye pafyumu na deodorants.
Utafiti umebaini kuwa zaidi ya asilimia 52 ya wanawake nchini hutumia vipodozi vyenye sumu ambavyo huwasababishia matatizo mbalimbali ikiwemo saratani ya ngozi,figo na kuharibika kwa mimba kwa Mama mjamzito.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Machi 29,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa