Halmashauri ya Manispaa ya Songea imepokea Vishikwambi 709 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya kugawa katika shule za Sekondari 25 na Shule za Msingi 82.
Hayo yamejili leo tarehe 04 Januari 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kuboresha utendaji kazi za kila siku na kuleta ufanisi pamoja na kupandisha taaluma.
Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala Wilaya ya Songea Pendo Daniel ambaye amewataka walimu hao kutumia Vishikwambi kwa matumizi sahihi ikiwemo na utunzaji wa kumbukumbu za shule.
Pendo alisema Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Vishwambi kwa Walimu ili kuboresha utendaji wa kazi hususani utunzaji wa takwimu sahihi za idadi ya wanafunzi, miundombinu ya shule, na matumizi mengine ya kiuhasibu.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Frederick Sagamiko amewataka maafisa Elimu Msingi na Sekondari kutenga bajeti kwa ajili ya kununua Vishikwambi kwa shule mpya zitakazokuwa zimejengwa.
Walimu nao kwa nyakati tofauti wamepaza sauti zao kwa kuishukuru serikali kwa kuwapatia vitendea kazi ambavyo wameahidi kuvitunza na kutunzia taarifa sahihi za shule.
Imeandaliwa na;
AMINA PILLY
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa