VITUO VYA ELIMU VISIVYOSAJIRIWA MARUFUKU
HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea imewaandikia barua wamiliki wote wa vituo vya kutolea elimu yoyote bila kusajiliwa kuacha mara moja kwa kuwa ni kinyume cha sheria na wanaweza kuchukuliwa hatua.Idara ya Elimu katika Manispaa hiyo imetoa maagizo kwa wataratibu wa elimu kata zote 21 kusimamia utekelezaji wa agizo hilo ambapo kuanzia Septemba 2017 hairuhusiwi mmiliki wa shule au kituo cha tuition kutoa masomo bila kusajiliwa.
Idara hiyo imebainisha kuwa zimeibuka Taasisi zisizo rasmi na watu binafsi kuanzisha vituo vya elimu na kujitangaza kwa njia mbalimbali kwamba zinatoa masomo ya ngazi mbalimbali za elimu kuanzia chekechea, msingi, sekondari na vyuo.Vitendo vya kuanzisha vituo hivyo ni kinyume cha sheria,kanuni na taratibu kwa sababu kuanzisha shule au kituo kuna taratibu zake ikiwemo kupata usajili kisheria na kufuata taratibu nyingine zinazotolewa mara tu baada ya kupata usajiri.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknlojia hutoa taratibu na miongozo ya kufungua na kuendesha shule,vyuo na vituo vya elimu vya umma na watu binafsi kwa ajili ya kutoa elimu rasmi na isiyokuwa rasmi kwa wananchi.
Kwa mawasiliano hakikisha unaonana na Idara ya Elimu Manispaa ya Songea au kupitia Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima ambao wanatoa utaratbu wa jambo hili.
Taarifa imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari wa Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa