JAMII ya viwavi jeshi aina ya Fally arm worms ambao waliingia katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma tangu Desemba 2017 na kufanya uharibifu wa mazao wamedhibitiwa kwa asilimia 95.
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Zawadi Nguaro amesema viwavi hao wana uwezo wa kushambulia aina 80 ya mazao yakiwemo mahindi,miwa na mtama na kwamba tangu wamelipoingia katika Manispaa hiyo walikuwa wanashambulia nyasi.
Hata hivyo anasema wadudu hao waligundulika mwishoni mwa Desemba 2017 wakiwa wameshambulia hekta zaidi ya 1000 za mahindi,wadudu hao hutoboa majani ya mahindi na kuchana kama kamba na kwamba wana uwezo wa kushambulia kwa kasi kubwa iwapo hatawadhibitiwa haraka.
Anayataja maeneo ambayo yaliathirika zaidi na wadudu hao kuwa ni Kata ya Lilambo ambayo hekta 299 ziliharibiwa,Subira(250),Tanga(180),Mletele(100),Ruhuwiko(120)Mshangano(50),Matogoro(10),Ruvuma(26),Seedfarm(20) na Mateka hekta tano.
Nguaro anasema tangu walipogundulika wadudu hao Idara ya kilimo imekuwa inatoa elimu na ushauri namna ya kupambana na ugonjwa huo ikiwemo viuatilifu vya kukabiliana na ugonjwa huo ambapo wakulima wamekubali ushauri na kununua viuatilifu hivyo kufanikiwa kupunguza tatizo hilo kwa kiwango kikubwa.
Anavitaja viuatilifu ambavyo vinatumika kukabiliana na wadudu hao kuwa ni MUPA FORCE 720 EC,AGROCRON 720EC,PROTRIN 600 EC,PROSPER 720 EC na DUDUBA 720 EC.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa