Uchaguzi mkuu ni jambo la msingi sana katika Taifa letu kwani ndipo tunapopata viongozi wanaobeba dhamana ya kutuongoza katika mapambano ya kiuchumi na jamii ili kuweza kutimiza malengo mbalimbali ya serikali kwa wananchi wake.
Kauli hiyo imetamkwa na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda katika semina kwa waandishi wa habari Mkoani Ruvuma iliyofanyika katika ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma leo 21/10/2020.
Mwenda alisema “lengo la kikao hicho ni kukumbushana mambo mbalimbali yanayohusu rushwa kuhisiana na masuala ya uchaguzi ambao unatarajia kufanyika tarehe 28 oktoba mwaka huu.”
Alibainisha kuwa sheria ya uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010 ilitungwa kwa madhumuni ya kuweka kwa sheria itakayosimamia na kuratibu mapato na kudhibiti matumizi pamoja na gharama za uchaguzi kwa vyama vya siasa na wagombea ikiwa imeainishwa matendo yanayokatazwa.
Aliongeza kuwa madhumuni ya sheria na kanuni hizo ni pamoja na kudhibiti vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi na kupata viongozi kwa njia ya haki ambapo sheria hizo ni pamoja na katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania yam waka 1977, sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007, sheria ya uchaguzi wa kitaifa namba 1 ya mwaka 1985 na kanuni zake, sheria ya gharama za uchaguzi namba 6 ya 2010, sheria ya mwenendo wa makossa ya jinai sura ya 20, sheria ya ushahidi sura 6, na hukumu za kesi zilikwisha tolewa maamuzi na mahakama.
Akizitaja sababu za kuwepo kwa rushwa katika uchaguzi ambapo hutofautiana kati ya wapiga kura na wagombea ambazo ni pamoja na wapiga kura- kuwa na tamaa ya kupata kitu chochote chenye kunufaisha bila ya watu wote, uelewa mdogo wa wapiga kura kuhusu haki na wajibu wao katika uchaguzi na umuhimu wa kura zao, umaskini unaosababisha kudai au kupokea rushwa, kukosa uzalendo, mazoea na utamaduni uliojengeka wakati wa uchaguzi ni ni sehemu ya kupata fedha na mmomonyoko wa maadili.
Aliongeza kuwa sababu za wagombea kutoa rushwa ni pamoja na utamaduni uliojengeka na kutojiamini nafasi aliyogombea kwa kutotoa kitu chochote hatachaguliwa katika uchaguzi, kuhofia kushindwa katika uchaguzi mkubwa na kutokubali kushindwa, na ukosefu wa maadili.
Hakusita kutaja madhara ya rushwa katika uchaguzi ni kukosa viongozi wazuri ambao ni wazalendo kwa Taifa letu, kupata viongozi wasio wazalendo wanaoingia madarakani kwa rushwa, kupata viongozi ambao wanalenga kurudisha gharama walizotoa kuingia madarakani, kutosimamia kikamilifu kwenye miradi ya maendeleo kutokana na kukosa viongozi wenye uchungu nayo, kudumaa kwa uchumi wa Taifa, kudidimiza haki ya usawa wa kushiika nafasi za uongozi, kudhoofisha demokrasia, kuondoa uhuru wa mpiga kura.
Alisema wajibu wa mwandishi wa habari katika kuzuia na kupambana na rushwa katika uchaguzi mkuu ni kufanya kazi kwa uadilifu, kuwa mtu wa kujielimisha mambo mbalimbali yanayokuzunguka, mwanahabari anawajibika kutoa taarifa ofisi ya TAKUKURU pale aonapo vitendo vya rushwa vinatokea, ni wajibu wake kukataa kuandika habari zinazokiuka maadili ya uandishi wa habari, na kushiriki mikutano ya kampeni ili kujua sera za vyama zitakazomwezesha kuchagua kiongozi atakaye wajibika katika jamii.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
21 OKTOBA 2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa