Halmashauri ya Manispaa ya Songea inaendelea kutekeleza mimakati ya kuboresha elimu kwa shule za Msingi na Sekondari katika kutatua changamoto za miundombinu ya Elimu ikiwemo na viti na madawati, pamoja na upatikanaji wa chakula shuleni.
Manispaa ya songea ina jumla ya wanafunzi 19,097 katika shule za Serikali 25 zilizopo Manispaa ya Songea, ambapo hali halisi ya mahitaji ya viti na meza ni 16,119 na upungufu ni viti na meza 3622.
Hayo yamejiri wakati wa kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika tarehe 22 Agosti 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kilichoshirikisha Waheshimiwa Madiwani wa kata zote 21, Maafisa watendaji wa kata 21, Maafisa Elimu, Wenyeviti wa Bodi za shule, pamoja na maafisa Elimu kata kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali za shule za Sekondari.
Akizungumza Naibu Meya Jeremiah Mlembe kwa niaba ya Mstahiki Meya Manispaa ya Songea amewataka Maafisa Elimu Kata, Maafisa watendaji wa kata pamoja na Madiwani kuhakikisha wanahamasisha wazazi kuchangia viti na meza kama walivyofanikiwa kata ya Matogoro ambao walivyoweza kuhamasisha michango kwa wazazi na kufanikisha kutanzua changamoto za madawati iliyokuwa inazikabili shule za kata hiyo.
Jeremiah amebainisha baadhi ya mikakati ambayo inakwenda kutekeleza ili kufikia lengo la madawati 3622 ni pamoja na bodi za shule kuitisha vikao vya wadau wa elimu, kuwepo kwa sheria ndogo pamoja na maelekezo mbalimbali yatakayotolewa kwa ajili utekelezaji huo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Songea Alto Liwolelu alisema “ hatua hiyo imekuja baada ya mafanikio kupitia mchakato uliofanywa na uongozi wa kata ya Matogoro ambao wamefanikiwa kutengeneza madawati zaidi ya 500 kwa shule za Serikali, hivyo amewataka viongozi kuiga mfano huo. “ Alipongeza”
Imeandaliwa
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa