Mstahiki Meya Manispaa ya Songea ameketi na wadau wa Maendeleo waliopo Manispaa ya Songea kwa lengo la kuweka mikakati rafiki ya uwekezaji katika Mji wa Songea.
Hayo yamejiri tarehe 25 Agosti 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kukuza uchumi na uwekezaji katika sekta ya ujenzi wa nyumba za kulala wageni, Hoteli, Bar, Kumbi za mikutano pamoja na nyumba za kupangisha.
Kikao hicho kilishirikisha wadau mbalimbali ikiwemo na Benki, Wafanyabiashara, viongozi wa vyama vya siasa, na wataalamu kwa lengo la kukabiliana na ongezeko la wageni ambao huhitaji kupata chakula na marazi ( Hoteli)
Kikao hicho kitafanyika tena mwezi Septemba 2023 kwa ajili ya kupata mrejesho wa makubaliano ya kikao hicho.
Imeandaliwa na;
Amina pilly
Kitengo cha mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa