UMOJA wa wafanyabiashara wa masoko Manispaa ya Songea (UWABIMASO) umetoa malalamiko juu ya uboreshaji wa miundo mbinu soko la Manzese (A).
Katibu wa soko hilo Hamisi Amiri Mapunda akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake ameitaja changamoto kubwa inayowakabili ni uchakavu wa vibanda vya kufanyia biashara ambapo wafanyabiashara hao wanasita kufanya marekebisho kutokana na tetesi kutoka Manispaa kuwa wanampango wa kuboresha soko hilo.
“Halmashauri ya Manispaa ya songea itoe taarifa iliyokamili juu ya uboreshaji wa vibanda hivyo ili tuwe na uhakika wa biashara zetu” amesema Mapunda.
Kwa upande wake Mhasibu wa soko hilo Shukurani Mapunda amesema kuwa pesa zinazokusanywa zinatumika kuendesha shughuli za soko kama kuwalipa wafanya usafi ,walinzi na makarani kwani shughuli hizo huendeshwa na wafanyabiashara na sio Serikali.
Soko la Manzese ni miongoni mwa masoko makubwa katika Manispaa ya Songea ambalo hutoa huduma mbalimbali kama kuuza samaki, nyanya , machungwa ,karoti ,vitunguu na bidhaa nyingine nyingi katika soko hilo.
Imeandaliwa na
Severine fussi
wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Agosti 16, 2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa