AFISA Biashara wa Halmashauri ya Manispaa Songea mkoani Ruvuma Furaha Mwangakala amewataka wafanyabiashara kukata na kulipia leseni kwa wakati ili kuepuka usumbufu wa kufungiwa biashara zao.
Mwangakala akizungumza ofisini kwake mjini Songea, ameeleza umuhimu wa kuwa na leseni ya biashara na kulipia kwa wakati na kwamba ni dhamana kwa mfanyabiashara,pia inatambulisha biashara yake, Serikali inamtambua na inamrasimisha mfanyabiashra na kazi yake.
Amesema kuwa ni muhimu kwa wafanyabishara kukata leseni kwa wakati ili kuepuka adhabu mbalimbali zinazoweza kusababisha kufungiwa biashara zao na kutokuwa huru katika utendaji wa kuuza na kutoa huduma ambapo kwa mfanyabiashara asiye na kibali na asiye lipia adhabu ya kisheria ni kati ya shilingi 200,000 na isiyozidi shilingi 1,000,000 .
“kwa mfanyabiashara leseni ni kama dhamana na anatakiwa kulipia leseni siku 21 mara baada ya kuisha.”amesisitiza Mwangakala
Hata hivyo amezitaja changamoto ambazo wanakumbana nazo ni pamoja na uelewa mdogo kwa wafanyabiashara na kusababisha wengi wao kutokuwa na leseni ambapo kwa mwaka 2018 wafanyabiashara wenye leseni walikuwa asilimia 96 na mwaka 2019 ni asilimia 94 hivyo kuna upungufu wa asilimia 2 kwa mwaka 2019.
Mwangakala amesema mwaka 2019 wafanyabiashara 96 wamefunga biashara zao kutokana na kufirisika hivyo kusababisha kupungua kwa walipaji kodi kwa asilimia mbili pia ameiomba serikali kuboresha gharama za kodi ili ziwe rafiki kwa wafanyabiashara.
Amezitaja namna mbili za kutoa leseni ambazo ni kwa bidhaa au huduma ambazo hudumu kwa mwaka na leseni za vilevi ambazo hudumu kwa mienzi sita.
Imeandaliwa na
Myovela Jamila
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Agosti 23, 2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa