Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali. Ahmed Abbas Ahmed amewataka wafanyabiashara Mkoani Ruvuma kutoa maoni yao kupitia kikao cha Tume ya maboresho ya Kodi kwa lengo la kufanyia ufumbuzi ili Serikali iweze kufanya kazi kwa ufanisi . Alisema mtakumbuka tarehe 04 Oktoba 2024 Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alianzisha Tume ya Maboresho ya Kodi kwa lengo lka kukusanya maoni ya wadau na wanyabiashara Nchini.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea tarehe 07 Februari 2025 ambacho kilihusisha wadau mbalimbali, pamoja na wafanyabiashara huku akiwataka kutoa maoni yao.
Akizungumza Makamu wa Tume ya Maboresho Ya Kodi Balozi Maimuna Tarishi alisema lengo la kuunda tume hiyo ni kukusanya maoni ya wadau nchini ili kusikiliza malalamiko ya muda mrefu kuhusiana na mfumo wa ulipaji wa kodi nchini.
Miongoni mwa changamoto zinazowasilishwa ni pamoja na utitili wa kodi, mamlaka nyingi za ukusanyaji wa kodi yenyewe pamoja na utaratibu wa kuafuatilia ulipaji wa kodi
Wakizungumza wafanyabiashara hao kikaoni hapo waliishukuru Serikali kwa kuanzisha mfumo huo ambao utasaidia namna ya ulipaji wa kodi.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa