MKUU wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amesema wafugaji zaidi ya 4oo wamevamia Hifadhi ya Gesimasowa iliyopo Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma ambapo serikali ipo katika mpango wa kuwaondoa wafugaji hao ndani ya hifadhi hiyo ambayo ni mazalia ya samaki adimu wa mbasa na Mbelele.
Mgema alikuwa anazungumza katika kikao cha kamati ya ushauri wilaya ya Songea ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea na kushirikisha wadau toka Halmashauri zote tatu za Madaba,Halmashauri ya Wilaya ya Songea na Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa