Wajasiriamali wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea wametoa wito kwa wanajamii kutambua umuhimu wa maadhimisho ya maonesho ya nane nane ambayo hufanyika kila mwaka nchi nzima.
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Salum Mkwamba, akizungumza katika viwanja vya maonesho ya Nane Nane Msamala mjini Songea, amewataka wanajamii kuwa na mwamko wa kushiriki katika maonesho hayo ili waweze kujipatia fursa mbalimbali zitakazowasaidia kujikwamua kiuchumi.
“tunawaomba wakulima kushiriki kwa wingi katika maonesho haya kwa kuwa wao ndio walengwa zaidi.” Amesema Mkwamba.
Kwa upande wake, mjasiliamali wa kikundi cha HEKIMA PRODUCTS SEED FARM “B” Flora Luena ameeleza uwepo wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na mazao na kuwaomba waananchi kufika katika maonesho hayo ili kujipatia bidhaa.
Hata hivyo Luena amezitaja changamoto kwa jamii kuwa ni kutotambua umuhimu wa Nane Nane hivyo kusababisha kukosa elimu ya ujasiriamali.
Naye, Mjasiliamali Mary Whine amewataka wakulima wapate mwamko wa kushiriki kwenye madhimisho ya Nane Nane na kuishukuru Serikali kwa kutambua umhimu wa ujasiriamali kwa kuwapatia mikopo na kuwaomba waendelee kuboresha zaidi mikopo hiyo ili iwafikie watu wengi.
Maonesho ya Nane Nane hufanyika kila mwaka kuanzia Agosti Mosi na kilele chake ni Agosti nane ambapo katika Manispaa ya Songea maonesho hayo hufanyika kwenye viwanja vya nane nane Msamala.
Imeandaliwa na
Elika Mwakinandi
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Agosti 5,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa