Mwenyekiti wa kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma wilaya ya Songea amefurahishwa na juhudiza utendaji kazi ya ujenzi wa kituo cha Afya katika kata ya Ruvuma.
Akitoa taarifa Mganga Mkuu wa Halimashauri ya Manispaa ya Songea, Dkt Mamerita Basikeamesema Manispaa ya Songea ilipokea fedha kutoka Serikali ya jamhuri ya Muungano waTanzania Shilingi milioni 400,kwa ujenzi wa kituo cha Afya Ruvuma mwezi Juni 24,2018.
Kwa upande wake Basike amesema Ujenzi wa kituo cha Afya cha Ruvuma ulianza Julai 24,2018 baada ya kupata mchoro kutoka OR-TAMISEMI.
Mradi huu umekamilika kwa kazi zote ambazo ziliainishwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI,mradi umegharimu shilingi Bilioni 400,
Basike amezitaja kazi zilizofanyika katika kumilika ni Jengo la OPD, Jengo la Maternity, Jengola Theatre, Jengo la Maabara, ujenzi wa shimo la choo na shimo la kongo la nyuma na ujenzi wa
kichomea taka.
“Halmashauri imeomba vifaa na madawati kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI ili kituo cha Afyakianze kutumika kituo hiki kitahudumia wananchi wa kata ya Ruvuma,Mateka, Majengo, subira,
Mfaranyaki na Lizaboni.”amesema Basike.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mdeme ameshauri wajenge baranara zenye lamiili kuondo vumi katika eneo hilo la kituo cha Afya kuondo mazingira ya vumbi kwa wagonjwa.
Ruvuma ni miongoni mwa kata 21 zilizopo katika Manispaa ya Songea.Kata hii ina jumla yamitaa minne ambayo ni Ruvuma Juu, Ruvuma Chini Mbulani A na Mbulani B kata ina jumla ya
wakazi 27,398 na shughuri za uchumi unaofanyika katika kata hiyo ni ufugaji na biashara
ndogo ndogo.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa