WALIMU wa shule za Msingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wameshauri wananchi kutambua umuhimu wa alama za barabarani ili kupunguza ajali.
Akizungumza wakati anawavusha wanafunzi wa shule ya msingi Songea,Mwalimu wa shule hiyo Pita Naneka amesema kuwa alama za vivuko vya waenda kwa miguu vimesaidia kupunguza ajali za barabani na kuepusha serikali kupata hasara zinazotokana na majeruhi na vifo vinavyotokana na ajali.
Mwalimu Naneka ameiomba Serikali ishirikiane na Polisi wa usalama barabarani kutoa elimu kwa wanajamii ili kutambua umuhimu wa alama za barabani, pia ametoa wito kwa madereva kufuata alama hizo ambazo zimewekwa katika maandishi angavu na sheria kali zichukuliwe kwa madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani.
“Wavuka wa miguu wanatakiwa kutambua alama ya pundamilia ni sehemu maalum ya kivuko cha waenda kwa miguu.”Amesisitiza Naneka.
Kwa upande wake Mwalimu Leonard Nkoma anayefundisha katika shule ya Msingi Songea amekiri kuwa alama hizo zimewasaidia wanafunzi kuwa salama kwa kuwa wanafunzi wanakuwa huru wanapovuka barabara na kufika shuleni kwa wakati .
Alama za barabarani ni vyema zikafuatwa ili kupunguza ajali za barabarini na kunusuru maisha ya watu na mali zao.
Imeandaliwa na
Severine Fussi
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Agosti 26, 2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa