Ni kutolewa kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa shule za Msingi na Sekondari Manispaa ya Songea yaliyotolewa kwa lengo la kufundisha wanafunzi kwa ajili ya kuwapatia fursa wanafunzi na kuweza kuonyesha vipaji vyao.
Mafunzo hayo ya michezo yameratibiwa na ofisi ya Mkoa wa Ruvuma kwa usimamizi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea yaliyofundishwa na wakufunzi kutoka chuo cha maendeleo ya michezo MALYA-Mwanza kuanzia tarehe 6 hadi 9 machi 2021 katika ukumbi wa chuo cha Ualimu Matogoro Songea Mjini.
Afisa michezo Manispaa ya Songea Mohamedi Kitesi alisema lengo mahususi la mafunzo hayo ni kufikia lengo la Serikali na kuhakikisha linazalisha kizazi imara katika michezo.
Kitesi aliongeza kuwa kama Halmashauri imejipanga kuendeleza kutetea ubingwa wa UMISETA na UMITASHUTA.
Ambapo mafunzo hayo yametolewa kwa washiriki 208 ambao ni walimu wa shule za msingi na Sekondari na kupatia fursa ya kujifunza aina ya michezo 7 ikiwemo na mafunzo ya ualimu wa michezo, pamoja na mafunzo ya waamuzi wa michezo kama wa mpira miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, riadha, mpira wa mikono na mpira kengere.
Washiriki wa mafunzo wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti ambapo walisema “wanaishukuru Serikali kwa kuwapatia mafunzo na kurejesha michezo shuleni kwani inasaidaia kujenga afya ya mwili, ajira kwa vijana, na burudani pia itawasaidia kuwashawishi wanafunzi kupenda masomo kutokana na uwepo wa michezo shuleni.”
IMERIPOTIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
10.03.2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa