KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dk.Laurian Ndumbaro amesema kuanzia Novemba mwaka huu serikali inaanza kutoa maslahi ya watumishi,ajira mpya na uhamisho.Akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Songea Dk.Ndumbaro amesema baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa watumishi sasa utekelezaji wa maslahi ya watumishi ikiwemo kupandishwa vyeo utekelezaji unaanza.
Naye Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora amewatahadharisha watumishi wa umma nchini kuhakikisha tarehe zao za kuajiriwa zipo sahihi ili kuepukana na kuondolewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao sasa umeboreshwa.Amesema kutokana na uboreshaji huo,hivi sasa kila siku inapofika saa sita usiku Mtumishi wa umma aliyefikisha miaka 60 anaondolewa mara moja kwenye mfumo wa malipo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akiambatana na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali watu wamefanya ziara katika mkoa wa Ruvuma kwa kutembelea wilaya zote za mkoa wa Ruvuma na kuzungumza na watumishi wa umma.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa