Halmashauri ya Manispaa ya Songea inatekeleza zoezi la umezeshaji dawa za minyoo na kichocho kwa wanafunzi wa shule za msingi 96 zilizopo Manispaa ya Songea ambalo linaendeshwa na Walimu wa afya chini ya usimamizi wa Wataalamu wa afya kuanzia leo tarehe 17 hadi tarehe 18 Novemba 2022.
Mratibu Elimu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Bload Komba alisema Manispaa ya Songea imeanza zoezi la umezeshaji wa dawa za minyoo na kichocho kwa wananfunzi wa shule ya msingi kuanzia miaka 5 hadi 14 kwa idadi ya wanafunzi 54,890 wakiwemo wavulana 27,426 na wasichana 27,710.
Bload alisema lengo la kutoa dawa hizo ni kwa ajili ya kinga ya minyoo tumbo na ugonjwa wa kichocho ambapo mwanafunzi atapimwa urefu kuanzia sentimita 90 ataweza kumeza dawa na endapo atakuwa chini sentimita 90 au chini ya iaka mitano 5 hatapewa dawa.
Alisema dawa itakayotolewa kwa wanafunzi ni dawa aina ya Albendazole - dawa za minyoo ya tumbo na dawa ya kichocho ambayo imeshauriwa kuanza kula chakula kabla ya kumeza dawa.
Aliongeza kuwa dawa hizo ni kinga na salama na hazina madhara endapo zitatumika kwa usahihi japokuwa yapo baadhi ya maudhi madogo madogo yanayoweza kutokea na ya muda mfupi ikiwemo na kichefuchefu, kuharisha, kichwa kuuma, homa, na maumivu ya tumbo endapo yatatokea maudhi madogo madogo watoe taarifa kwa wataalamu wa afya kwa hatua zaidi .
Akibainisha Manufaa ya dawa za kinga tiba endapo zitatumika kwa usahihi ni pamoja na kupunguza maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, kuua vimelea vya magonjwa hayo, kuepusha upungufu wadamu, kupunguza magonjwa ya ngozi, kuboresha nguvu kazi pamoja na kuwafanya watoto wakue vizuri. “Alibainisha “
Amewataka walimu hao kusimamia zoezi hilo kwa weredi na kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa na wataalamu wa Afya na kuhakikisha wanafunzi walioandikishwa wote wenye umri kuanzia miaka 5 hadi 14 wanapewa dawa za kinga tiba.
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa