Manispaa ya Songea ni miongoni mwa Halmashauri nane zilizopo Mkoani Ruvuma ambazo zitashiriki mashindano ya ubunifu wa Sayansi na Teknolojia kwa wanafunzi wa shule za Sekondari nchini.
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Songea Devotha Luwungo amesema Halmashauri ya Manispaa ya Songea ina jumla ya Sekondari 41, kati ya hizo shule za Sekondari 3 ndizo zilizofanya vizuri kwa ubunifu wa vipaji vya wanafunzi ambazo ni Matarawe Sekondari, Zimanimoto Sekondari, na Matogoro Sekondari.
Devotha alieza kuwa mashindano hayo yatahusishwa na uibuaji wa vipaji maalumu vya Sayansi na Teknolojia ambapo kwa Manispaa ya Songea imepata wanafunzi 3 wenye vipaji bora ambao ni Abdul Omari Msafiri mwanafunzi kutoka shule ya Zimanimoto Sekondari – muundaji wa kifaa kinachotenganisha vimiminika vigumu na laini ( mfano mafuta kutoka kwenye maji) improvised separating funnel, mwanafunzi Walen John Mbunda kutoka shule ya Sekondari matarawe - uundaji wa magari yanayotumia umeme ( auto mobile), na mwanafunzi Annastasia Leonard Mdogi kutoka shule ya sekondari ya Matogoro-mchoraji wa picha mbalimbali.
Naye Mkuu wa shule ya sekondari Matarawe Francis Sasu alisema mwanafunzi Walen John Mbunda ni mwanafunzi wa kidato cha tatu ambaye aliwahi kushiriki mashindano ya Majimaji Selebuka mwaka 2020 na alionyesha kivutio cha kipaji kikubwa, na hadi leo hii ameweza kufanya vizuri kwa kubuni uundaji wa gari linalotumia umeme (auto mobile).
Alisema “mara nyingi huwa wanawahimiza wanafunzi kuhusu mitaala ya kawaida na kuwashawishi, kuwashauri juu ya vipaji vyao mbalimbali pamoja na kuwatia moyo ili waweze kukuza vipaji vyao kwa sababu yawezekana mtoto akawa na uwezo mdogo wa kitaaluma darasani lakini akaweza kuwa na kipaji kizuri cha ubunifu”. Sasu alibainisha.
Nao wanafunzi washiriki wa mashindano hayo, walisema wanaiomba serikali iwasaidie kuwawezesha kuwapeleka kusoma shule zenye vipaji maalumu ili waweze kuboresha fani zao.
Akizitaja faida za kutumia magari yasiyotumia mafuta ni pamoja na kuokoa gharama za mafuta, kuondoa uchafuzi wa mazingira (moshi) na nyinginezo. “Alibainisha mwanafunzi Walen John Mbunda.”
Mashindano hayo yamemalizika kiwilaya na sasa yataendelea kufanyika ngazi ya mkoa na hati;maye kitaifa.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
10.02.2021.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa