WANAHABARI 27 kutoka Tanzania Bara na Visiwani wamechaguliwa kushiriki katika mafunzo ya ubobezi katika habari za mazingira.
Mafunzo hayo ambayo yameratibiwa na Umoja wa Klabu wa wanahabari Tanzania (UTPC) yanafanyika kwa siku tano kwenye ukumbi wa Kings Way mjini Morogoro chini ya Mkufunzi Mbobezi katika masuala ya mazingira Deogratius Mfugale.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo Afisa program wa Kitengo cha Mafunzo na Utafiti wa UTPC Mkao Makuu jijini Mwanza Victor Maleko amesema lengo ya kufadhili mafunzo hayo kwa wnahabari nchini,ni kuhakikisha kuwa inajengwa timu ya wanahabari wabobezi katika mazingira.
Amesema anamatumaini makubwa kuwa mara baada ya mafunzo hayo,wanahabari sasa wataandika habari ambazo zinaleta mabadiliko na matokeo chanya katika sekta ya mazingira ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo Deogratius Mfugale amelitaja lengo la kozi hiyo ni kuwajengea uwezo wanahabari ili kutambua kutambua uhusiano uliopo kati ya binadamu,mazingira na maendeleo.
“Wanahabari wanatakiwa kujijengea uhalali wa kuitwa waandishi wa habari kwa kufanya habari zinazoleta mabadiliko na matokeo chanya kwa kufanya uchambuzi badala ya kuendelea kuripoti matukio ambayo yanaripotiwa kwenye mitandao ya kijamii na watu ambao sio wanahabari’’,anasisitiza Mfugale.
UTPC kupitia Mpango Mkakati wake wa 2016 hadi 2020 unatekeleza moja ya malengo yake kwa kutoa mafunzo kwa wanachama wa vyama vya wanahabari nchini.
Imeandikwa na Albano Midelo
albano.midelo@gmail.com,simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa