Uongozi wa Kata ya Mwengemshindo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma umeishukuru serikali kwa kuwapatia huduma ya maji ambayo hawajawahi kupata tangu uhuru.
Diwani wa Kata hiyo Osimund Kapinga akizungumza baada ya Kamati ya siasa ya CCM kutembelea mradi huo,amesema kwa miaka mingi akinamama walikuwa wanasafiri umbali mrefu kutafuta maji ambayo sio safi na salama ambapo hivi sasa changamoto hiyo imepatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Kapinga amesema upatikanaji wa maji ulikuwa ni mgumu sana na kusababisha matatizo ya kiafya kutokana na kutembea kwa umbali mrefu kufuata maji na pia kutumia maji yasiyo salama kutoka kwenye visima vilivyochimbwa kwenye mabonde na visvyo na ulinzi wowote kwa kuangalia usafi na usalama wa maji hayo.
“kwa kweli hatuna budi kusema asante kwa msaada huu wa maji.” Amesema Kapinga
Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Songea Mhandisi Samwel Sanya aameiambia Kamati hiyo ya siasa kuwa mradi huo uliibuliwa na wananchi wenyewe katika mwaka wa fedha 2016/2017 na kukamilika 2018/2019 .
Kulingana na Sanya mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 490 ambazo zimetumika katika ujenzi wa miundombinu ya maji na ununuzi na ufungaji wa mfumo wa mionzi ya jua na kwamba fedha zote za ujenzi wa mradi zimetoka serikali kuu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho amewaomba wanachi kuthamini na kutunza mradi huu kwa kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu pia amewaagiza wataalam kuendelea kufanya marekebisho ya mradi huo ili kuboresha huduma hiyo.
Mtaa wa Luhila Kati ni mojawapo katika Mitaa kumi ya awali ambayo imetekeleza ujenzi wa miundombinu ya maji.
Imeandaliwa na
Bacilius Kumburu
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Agosti 29, 2019.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa