• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI Ruvuma wampongeza RPC kwa kukomesha uhalifu

Tarehe ya kuwekwa: July 14th, 2019

Wananchi wa Kata ya Mpepo Wilayani Nyasa,  wamempongeza Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Ruvuma Simon  Maigwa, kwa kuwakikishia usalama wa mali na maisha licha ya kuishi Karibu na mpaka wa Tanzania na Msumbiji.

Wananchi hao, wametoa pongezi kwa kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma, katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Lunyele kata ya Mpepo Wilayani Nyasa hivi karibuni. Mkutano aliokuwa na lengo la kuimarisha ulinzi shirikishi katika eneo la mpakani mwa Nchi ya Tanzania na Msumbiji.

Wananchi hao walifafanua kuwa awali, kulikuwa na matukio yaliyokuwa yakiwapa hofu ya kufanya kazi zao, kwa kuwa  ilikuwa haiwezekani kwenda hata kulima shambani,  lakini mara baada ya kuimarisha Ulinzi na Usalama, sasa wanafanya kazi zao kwa amani, na kumtaka Kamanda huyo kuwapa kibali cha kujenga kituo cha Polisi katika Tarafa ya Mpepo ili kuweza kukabiliana na matukio ya kihalifu katika Tarafa ya Mpepo kwa kuwa ni  tarafa inayopakana na Nchi jirani Ya Msumbiji.

Wananchi hao waliongeza kuwa wana imani na kamanda huyo, kwa kuwa tukio linapotokea huwa anakuja mwenyewe, bila kutuma mwakilishi na hata leo katika mkutano wa kuimarisha ulinzi shirikishi na usalama wewe mwenyewe umekuja.

“Kamanda wa Polisi sisi tuna imani kubwa  sana na wewe kwa kuwa kila mara umekuwa pamoja na sisi bila kutuma mwakilishi unafika wewe mwenyewe. sisi sote uliyozungumza tumeyaelewa na tutayafanyia kazi na tunakupongeza sana kwa juhudi zako za ufanyaji kazi wako alisema Kiliani Kumburu huku akishangiliwa na wananchi wengine” .

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma  simon Maigwa, Akiongea na wananchi hao katika mkutano huo wa hadhara, aliwahakikishia Usalama wa mali na maisha yao, na kuwataka wafanye kazi za kujenga taifa bila woga wowote kwa kuwa mkoa wa Ruvuma ni salama na hakuna tatizo lolote na atakayeingia kwa kujaribu kuhatarisha Usalama kamwe hataweza,na hatatoka salama.

Aliongeza kuwa kuhusu ombi la ujenzi wa kituo cha  polisi cha kisasa kitakachohudumia Tarafa ya Mpepo Wilayani hapa, amelipokea na hana pingamizi lolote na atashirikiana nao kwa hali na mali katika kutatua changamoto za ujenzi  huo, na atawaletea polisi na vifaa kwa ajili ya kuhakikisha jamii inakuwa salama muda wote na wanafanya kazi bila uoga wowote.

“Napenda kuwaeleza ndugu wananchi wa kata hii ya Mpepo kuwa Ruvuma ni salama kila mtu aendelee kufanya shughuli zake za kujiletea maendeleo,yeyote atakayejaribu kuingia na kujaribu kutishia amani wananchi kamwe, hatatoka salama. Na nimesikia mnahitaji kujenga kituo cha Polisi hakuna tatizo tushirikiane tujenge na mimi nitaleta Askari mara baada ya kujenga kituo cha kisasa cha polisi kataka kijiji cha tingi ambapo ni makao makuu ya Tarafa ya Mpepo”alisema kamanda Maigwa.

Aliongeza kuwa katika kila Kata ameleta polisi Kata ambaye anatakiwa Kuishi katika kata husika na kuhakikisha ulinzi na Usalama unaimarika kila kata.Hivyo aliwataka wamnanchi hao kushirikiana na Polisi kata aliyeletwa.

Aidha katika hatua nyingine aliendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Polisi, cha Tarafa ya Mpepo ambapo jumla ya shilingi laki mbili na ishirini na nne elfu (224,000/=) zilipatikana na kukabidhiwa kwa Ofisa Tarafa wa Tarafa ya Mpepo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Nyasa  Isabela Chilumba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika  Wilaya hii aliwataka wananchi kuhamasika na kujitoa kwa dhati kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha polisi kwa kila kaya kuchangia nguvu zao kwa kuwa, ulinzi ni muhimu sana katika jamii . kwa sasa kituo kilichokuwepo ni kidogo ambacho hakina uwezo wa kuhudumia Tarafa yote ya Mpepo.

Pia aliwataka viongozi wa serikali ya vitongoji, Kijiji, na Kata zote kuwa na Daftari la kusajli wageni wote wanaoingia ili kuweza kujua ni wahalifu au ni raia wema.

Imeandaliwa na Netho Sichali, Afisa habari wilaya ya Nyasa. 0767417597

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa